0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga.
Tanzania imesema mazungumzo yanaendelea ili kuibuka na makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC na Muungano wa Ulaya yatakayokuwa na maslahi kwa pande zote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga amesema hayo jijini New York, Marekani akisema kuwa wana jumla ya miezi minne ya kufanya mazungumzo hayo.
Balozi Mahinga amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni pamoja ni kuweza kuanisha malengo mapya ya Jumuiya pamoja mapungufu yaliyomo kwenye mkataba ili nchi zote ziweze kwenda sawa.
Aidha Balozi Mahiga amezungumzia suala la muungano wa Ulaya kutaka kuanza kutoza kodi bidhaa kutoka Kenya, na kusema kuwa wameshaongea na umoja huo kusubiri kwanza hadi pale watakapomaliza mazungumzo hayo.

Chapisha Maoni

 
Top