0
Waziri Mwigulu Nchemba akiwa ziarani mkoni Manyara
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba amesema serikali inatambua changamoto zote zinazozikabili taasisi za majeshi yaliyopo chini ya wizara yake na kwamba utatuzi wake unaendelea kufanyika.

Waziri Mwigulu amesema hayo mara baada ya kupata taarifa ya majengo ya ofisi, makazi na vitendea kazi katika Jeshi la Polisi, Zimamoto, Uhamiaji na Jeshi la Magereza mkoa wa Manyara.
Mhe. Mwigulu akiwa katika ziara yake ya siku moja katika mkoa huo amesema kuwa mambo ambayo yapo ndani ya bajeti watayashughulikia haraka iwezekanavyo ila hata ambayo yapo nje ya bajeti watafuatilia pia ili kuboresha sekta hiyo muhimu kwa ulinzi wa nchi na wananchi kwa Ujumla.
"Makazi, vitendea kazi na maslahi kwa wapiganaji wetu kwa serikali hii ya awamu ya tano tunakwenda kuacha alama. Tutatumia nguvu kazi tuliyonayo kuanzia wafungwa wenye sifa ya kufanya kazi,vikosi vya kazi kwenye majeshi na bajeti tunayoipanga kila mwaka kuhakikisha tunapata majawabu ya kudumu
Awali akitoa changamoto zinazowakabili Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara amesema kuwa mpaka sasa ofisi ya kamanda wa polisi ipo katika jengo la kuazima huku majengo mengine ya polisi yakiwa ni ya zamani na hakuna ofisi za kutosha.

Chapisha Maoni

 
Top