0

Hoteli ya SYL nchini Somalia
Image captionHoteli ya SYL nchini Somalia

Bomu kubwa limelipuka nje ya hoteli moja katikati ya Mogadishu karibu na lango la jumba la rais nchini humo.
Takriban watu 12 wameripotiwa kuuawa.Kundi la wapiganaji wa Alshabab limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Mtu mmoja aliyeshuhudia mlipuko huo amesema kuwa ameona watu wengi wakiwa wamejeruhiwa.Amesema kuwa hoteli hiyo imeharibika vibaya na kwamba vikosi vya usalama vimewasili katika eneo hilo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa mkutano wa usalama ulitarajiwa kufanyika katika hoteli hiyo ya SYL.
Hoteli hiyo imeshambuliwa mara kadhaa na al-Shabab katika miaka ya hivi karibuni..

Chapisha Maoni

 
Top