0
Sam Misago
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mtangazaji wa EATV, Sam Misago aliyeachia wimbo wake mpya ambao tayari umeshaibua minong'ono, kutokana na jina la wimbo huo.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Sam Misago amesema ataachia video yake mpya ya 'vyura na madanga' kadri ya sanaa yake inavyohitaji, na maudhui ya wimbo huo bila kuhofia rungu la BASATA, ambao wamekuwa wakifungia nyimbo za wasanii pale nyimbo zao zinapokuwa na matatizo kwenye maudhui yake.
"Mi nitatoa video ambayo director anataka video ya namna hiyo na mimi niridhishwe na video ya namna hiyo, kwa hiyo kama wataifungia wao ni sawa waifungie lakini nitahakikisha sanaa yangu ambayo nataka kuionesha kwenye hii ngoma na ujumbe umemfikia yule anayetaka kuiangalia video, kama ngoma ina magumashi basi video nayo lazima iwe na umagumashi, kwa sababu siwezi nikalazimisha kufanya video ambayo iko 'decent", alisema Sam Misago.
Sam Misago aliendelea kusema kuwa amefikia kufanya uamuzi huo kutokana na kwamba sanaa haina mipaka na huwezi kuiwekea sanaa mipaka.
"Sanaa haina mipaka, huwezi kuiwekea mipaka sanaa it doesnt matter who you are, kwa hiyo mimi kama sanaa yangu najua bwana kwenye 'vyura na madanga' inabidi niweke bebe flan hivi mkali, namuweka huyo bebe na ataonekana kwenye video, atakayesema bwana hii sanaa haitakiwi kwenye TV basi ataifungia ila sanaa haina mipaka, huwezi kuweka mipaka kwenye sanaa", alisema Sam Misago.

Chapisha Maoni

 
Top