0
Mkuu wa kitengo cha masuala ya watumiaji wa mitandao wa TCRA Isack Mruma
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewataka wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao kwani sheria ya uhalifu wa mitandao ya mwaka 2015 ipo na inafanya kazi yake.

Akizungumza katika kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV, Mhandisi wa mawasiliano kutoka TCRA Victoria Rulakara amesema kuwa wanaotumia vibaya mitandao kwa kuposti picha za utupu, sheria imeweka wazi kwamba watafungwa kifungo cha miaka 20 au kwenda jela miaka 7 au vyote kwa pamoja.
“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia pabaya, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema” Amesema Victoria
Kwa upande wake Mkuu wa itengo watumiaji wa mitandao Isack Mruma amesema TCRA wanaendelea na kampeni mpya ya kuelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao, kampeni ambayo itadumu kwa miezi mitatu.
Aidha Mruma amewataka wananchi kuacha kuanzisha tovuti zenye majina ya uongo kwa lengo la kuchochea au kuchafua watu wengine kwani , TCRA ina uwezo wa kuwabaini wote na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Chapisha Maoni

 
Top