0
Bei ya bidhaa muhimu ikiwemo vyakula imeendelea kuwa ya kawaida katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El Hajji, tofauti na ilivyozoeleka ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakitumia kipindi hiki kama fursa ya kupandisha bei za bidhaa zao.

UMBEA MFULULIZO imetembelea masoko kadhaa jijini Dar es Salaam na kukuta vyakula hasa vya jamii ya nafaka vikiuzwa kwa bei ya chini kama vile mchele ambao huuzwa kwa kati ya shilingi 1,200 na shilingi 2,000.
Hata hivyo bidhaa pekee iliyoonekana kuongezeka bei kidogo ni nyama ambapo katika mahojiano, wamiliki wa maduka ya kuuzia nyama wameihusisha hali hiyo na uhaba wa ng'ombe unaotokana na idadi kubwa ya mifugo hiyo kutumika kama sehemu ya ibada ya sikukuu ya Eid El Hajji ambayo huadhimishwa kwa kuchinja.

Chapisha Maoni

 
Top