0

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi.

Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchini Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahidi lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri.

Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta.

Lowassa alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akigombea kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA.

Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.

Akielezea Opersheni UKUTA, Lowassa alisema kuwa walipanga kuandamana ili kupinga dalili za udikteta alizoanza kuzionyesha Rais Magufuli.

Chapisha Maoni

 
Top