0

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Kenya itatoa msaada wa mabati, mablanketi na magodoro kwa Tanzania kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Jumamosi iliyopita katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Msaada unatarajiwa kuanza kuwasili kesho Jumanne kwa ndege za Jeshi la Anga la Kenya hadi mkoani Kagera ambao ndiyo mkoa ulioathrika zaidi.
Mapema leo, Rais Uhuru Kenyatta alimpigia simu Rais Dk. John Pombe Magufuli, kumpa pole na kueleza mshikamano wake na serikali ya Tanzania na wananchi wake kufuatia tetemeko hilo lililosababisha vifo vya watu, uharibifu wa mali, na majeruhi.
Rais Kenyatta amemwambia Rais Magufuli kwamba, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 16, mamia ya majeruhi ambao ni dada na kaka zao na kuongeza kwamba, kwa niaba ya serikali ya Kenya na wananchi wake, na kwa niaba yake binafsi amempa pole Rais Magufuli, serikali na wananchi wa Tanzania na hasa familia zilizoondokewa na wapendwa wao.
Rais Kenyatta amewatakia wote waliojeruhiwa wapone haraka na kuziombea familia zilizopteza ndugu jamaa na marafiki

Chapisha Maoni

 
Top