0

KR Muller amesema kama angetaka kurudi TMK Wanaume Family kwa Juma Nature angekuwa amerudi kwa kuwa hakuna aliyemfukuza.


Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo ‘Rada Entertainment’ kwa TID, ameiambia Bongo5 kuwa bado anafurahishwa na maisha mapya ndani ya Rada Entertainment.

“Mimi sijafukuzwa TMK, na pia naishi Temeke, kwa hiyo kama ningeamua kurudi TMK hakuna mtu ambaye angenifukuza kwa sababu sijafukuzwa,” alisema KR

Madai ya Juma Nature kuwa KR ameharibikiwa toka ajiunge na Rada ya TID, rapa huyo amekanusha na kudai yupo vizuri kabisa tofauti na watu wanavyosema.

“Kusema kweli mimi ni mtu mzima,na najitambua kwa hiyo swala la kusema TID ananiaribu siyo kweli kabisa,” alisema TID.

Chapisha Maoni

 
Top