0

Picha:Polis Kutoka Kenya Linda Okele Akiwa na vazi la Kubana Mwili lililozua Gumzo Nchini Huko
Naibu Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Abrahman Kaniki amewaagiza makamanda na maofisa waandamizi wa jeshi wa mikoa yote kuhakikisha wanasimamia nidhamu ya uvaaji kwa askari wa kike na kiume na watakaokutwa wamevaa sare zinazoonyesha sehemu za miili yao watachukuliwa hatua.


Akizungumza na askari hao wakati akifungua kongamano la siku 3 la mtandao wa polisi wanawake mjini Dodoma, Naibu IGP , Inspekta Jenerali huyo amepiga narufuku uvaaji wa sketi fupi kwa askari wa Jeshi hilo.

“Kwa wale wanaume, yeyote ambaye anavaa ‘kata k’ kamanda na kesi yakujibu, hivyo hivyo ma-WP ambao wanavaa kinyume na taratibu ambazo zipo jeshi la polisi kamanda ana kesi yakujibu, lakini itakwenda sambamba na yule in charge,” alisema Kaniki.

Pamoja na hilo amewaonya viongozi wa jeshi ambao wamekuwa wakivunja utaratibu , ikiwamo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na askari wa chini , kwa kuwa hiyo ni sawa na kumkabidhi mtu kondoo kuwachunga na badala yake akawala .

Chapisha Maoni

 
Top