Ubao wa matokeo wakati wa mechi kati ya Yanga na Majimaji, baada ya yanga kupata bao la 3, hivyo ulipaswa kusomeka 3-0 |
Akizungumza katika kipindi cha 5Sports cha EATV jana usiku, Afisa Habari wa shirikisho hilo Alfred Lucas amesema kuwa TFF siyo mmliki wa uwanja huo, hivyo haipaswi kubebeshwa mzigo wowote kuhusu mapungufu yanayolalamikiwa.
Amesema wao kama TFF walijiridhisha kuwa uwanja huo unaweza kuendelea kutumika kwa michuano hiyo baada ya kufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu, na sasa kuwa umekamilika.
Baadhi ya wadau wa soka wakiwemo wachezaji wamekuwa wakiulalamikia uwanja huo kuwa na mapungufu makubwa hasa katika eneo la kuchezea (Pitch) huku wengine wakishangazwa na hatua ya marekebisho yaliyofanyika kuwa ni ya majukwaani pekee huku eneo la kuchezea likiachwa kama lilivyokuwa.
Kasoro nyingine iliyobainishwa na kituo hiki, ni kutokuwepo kwa ubao wa kisasa wa matokeo (Score Borad) jambo linalosababisha usumbufu wa namna ya kuandika matokeo kwa njia ya kubandika kwa kutumia gundi (Cello Tape), na kuweka uwezekano mkubwa wa kukosewa kwa matokeo.
"Huo uwanja unamilikiwa na serikali, kwa hiyi kama kuna mapungufu kama hayo mnatakiwa kuwauliza wao, siyo TFF" Ilikuwa ni sehemu ya jibu la Alfred Lucas.
Lucas alitumia nafasi hiyo pia kutoa ufafanuzi kuhusu mechi ya Azam na Simba ambayo awali ilikuwa imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa, lakini kutokana na uwanja huo kuwa na ratiba nyingine, Lucas amesema kuwa mechi hiyo imehamishiwa katika uwanja wa Uhuru, katika tarehe ileile iliyopangwa ambayo ni Septemba 17, mwaka huu.
“Mechi ya Azam na Simba haijaahirishwa, iko pale pale katika tarehe iliyopangwa, mechi hiyo itachezwa tarehe 17 Septemba, 2016 katika uwanja wa Uhuru”
Alipoulizwa kuwa ni kwanini mechi isifanyike katika uwanja wa Chamazi kutokana na kwamba Azam ndiyo wenyeji, Lucas alipatwa kigugumizi na kusema kuwa hiyo ni mipango ambayo ilikwishafanyika kwahiyo haiwezi kubadilishwa.
Chapisha Maoni