0
Wanafurahia glasi ya Bia
Watafiti kutoka Uswizi wamethibitisha kwamba glasi moja ya bia inawafanya watu kujuana zaidi na kufunguka roho.
Kundi la watafiti kutoka hospitali ya Chuo Kikuu cha Basel wamefanyia utafiti watu 60, nusu wakapewa bia na wengine wakapewa kinywaji kingine, ambacho siyo bia. Kisha watu hao wakashiriki katika matukio tofauti tofauti.
Mtafiti mkuu Profesa Matthias Liechti amesema watu wanaokunywa bia kwa wastani ni wachangamvu, hutangamana na kujana vyema kuliko wale ambao hawakunywi bia. Pia imethibitishwa wanaokunywa bia hushirikiana kwa pamoja masuala mengi na pia bia inasaidia kutuliza mawazo, lakini lazima utumiaji wa mvinyo usiwe na kupindukia.
Mapema mwaka huu Serikali ya Uingereza ilitoa masharti mapya ya utumiaji wa mivinyo. Ushauri wa serikali ulipendekeza raia wasikunywe zaidi ya glasi saba za mvinyo au bia.
Masharti haya yalitolewa baada ya ushahidi kuonyesha kwamba unjwanji pombe kupindukia unahatarisha mtu kupata saratani ya matiti.
Lakini utafiti wa karibuni umesema mradi mtu kutumia bia kwa masitani basi utakua na furaha, na pia inazuia kujihusisha na ngono ya kiholela.

Chapisha Maoni

 
Top