Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeombwa kushirikiana na uongozi wa Kata ya Kawe, katika juhudi zake za kulitafutia ufumbuzi suala la ukosefu wa kituo cha mabasi ambacho imekuwa ni kilio kikubwa cha wakazi wa eneo hilo.
Kilio hicho kimekuwa pia kikitolewa na wafanyabiashara katika soko la Kawe ambao wamesema uwepo wa kituo hicho ungesaidia kuchangamsha biashara sokoni hapo.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo na Diwani wa Kawe Bw. Muta Lwakatare ambaye amesema kukosekana kwa kituo hicho kumekuwa na athari za kiuchumi kwa makundi mbalimbali, wakiwemo pia vijana waliojiajiri kupitia biashara ya bajaji na bodaboda.
Amesema kuwa mahali zinaposimama daladala hivi sasa siyo eneo rasmi kwani mbali ya kuikosesha manispaa mapato ambayo yangetokana na ushuru wa maegesho, imekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara kutokana na magari hayo ya abiria kuziba barabara.
Chapisha Maoni