0

Alikiba amedai kuwa collabo si kitu kilichopo kwenye menu yake.
Akiongea na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommmy kwenye red carpet za MTV MAMA jijini Johannesburg, Afrika Kusini Jumamosi iliyopita, aliyemuuliza iwapo ametumia fursa hiyo kuzungumza na wasanii mbalimbali wa Afrika kuhusu collabo, Kiba alidai kuwa mipango yake ni kufanya muziki mzuri.

“Hiyo sio focus yangu, focus yangu ni kufanya muziki mzuri,” alisema Alikiba.

Muimbaji huyo alikuwa ametajwa kuwania vipengele viwili akiwa na Sauti Sol kupitia wimbo wao Unconditionally Bae.

Chapisha Maoni

 
Top