0










Leo katika kanisa la Ufufuo na Uzima Yule askofu machachari Askofu
Gwajima amejibu mashambulizi ya hotuba ya RC wa Dar Es Salaam
yaliyofanyika television ya Star TV majuma kadhaa yaliyopita. Amechambua
hotuba yote aliyofanya RC pale Star TV, ameeleza elimu ya Nape Nnauye,
amechambua tukio la uvamizi pale Clouds FM na akaeleze uhalali wa jina
la Bashite Kwa RC. Askofu Gwajima ameshusha nondo zake za kutosha
kudhihirisha kuwa muhusika wa hotuba jina lake halali ni Bashite.
Ameenda mbali na kudai kuwa hata namba za simu za baba yake kwenye
miamala ya fedha zimesajiliwa kwa jina la Bashite. Na akaitaja namba
husika. Anasema kabla sakata halijapamba moto bila wao kushtukia aliruka
had mwanza na ana picha alizopiga kwenye rejesta za shule ya msingi na
sekondari na majina ya muhusika yalikuwa ni Bashite. Pia askofu Gwajima
anasema wiki iliyopita aliwasiliana na Anthony Diallo kumuuliza kwa nin
aliruhusu kipindi cha kumdhalilisha. Askofu anasema Mh Diallo alimjibu
kuwa aliweza kumruhusu kumpa kipindi kwa kuwa Bashite alimuambia kuwa
nataka kuonyesha vyeti kwa watanzania na hivyo Diallo akaona ni jambo
jema. Askofu anasema hata baada ya kipindi Mh Diallo alishangaa kwa
sababu Bashite hakufanya kama alivyoomba. Askofu akaonyesha ujumbe mfupi
wa simu uliotoka kwa Diallo.



Video:-



Chapisha Maoni

 
Top