Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewasihi Mabaharia na nahodha wa meli kushirikiana na Serikali kuwafichua wanaoingiza mizigo ya magendo na Dawa za Kulevya kupitia ukanda wa Bahari.
RC Makonda amesema hayo leo jijini Dar es salaam kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mabaharia ambapo amesema ushirikiano huo utasaidia kudhibiti uingizwaji wa mizigo ya magendo nchini.
Amesema kazi ya ubaharia ni kazi muhimu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Taifa kupitia ukanda wa Bahari hivyo Mabaharia wanapaswa kuona wanalo jukumu la kuchangia Ukuaji wa Pato la Taifa.
Aidha RC Makonda amewaahidi Mabaharia kuwa atamfikishia Rais Magufuli changamoto walizoainisha ikiwemo ya ugumu wa upatikanaji wa Ajira kwa mabaharia wazawa ugumu wa kupata Mafunzo kwenye meli, Ajira kwenye Meli za uchimbaji Mafuta na changamoto za Kisera na Sheria.
Kwa upande wake mmoja wa Mabaharia aliesoma Risala Bwana Aloyce Mpazi amesema watazidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha ukanda wa Bahari unakuwa moja ya nyanja zinazohusika kuchochea ukuaji wa Biashara.
Chapisha Maoni