0
Manispaa ya Kinondoni imefanya vizuri zaidi katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017 kwa kupata ufaulu wa asilimia 93.02, ambapo imekuwa halmashauri ya kwanza kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika sherehe za uzinduzi wa kukabidhi tuzo kwa shule na walimu waliofanya vizuri meya mstahiki wa kinondoni Benjamin Sitta kama manispaa wameamua kufanya hivyo ili kuwapa motisha walimu na shule ambazo zimefanya vibaya mwaka huu ziweze kujipanga ili zifanye vizuri,


Aidha kutokana na mafanikio hayo manispaa ya Kinondoni kwa kutambua mchango wa walimu imeamua kutoa tuzo kwa walimu wote ambao masomo yao yamefanya vizuri kwa kufaulisha alama "A", hivyo kila A moja mwalimu wa somo husika amepewa sh.2500 ikiwa ni mwanzo na motisha kwa walimu.


Hivyo shule zote 78 zilizopata ufaulu wa juu kwa mwaka 2017 zimepewa tuzo ili kuzihimiza shule zote kuongeza juhudi na kuimarisha ufaulu wao kwa kasi zaidi.

 " Nachukua fursa hii kuwapongeza walimu wote wa shule za msingi, wazazi mkurugenzi, afisa elimu na Rais kwa jitihada wanazozifanya kwa kufanikisha mpango wa elimu bure ambapo unapelekea kupata matunda haya" alisema Sitta.

Kwa upende wake mkuu wa wilaya hiyo Ally Hapi amewapongeza walimu wote ambao shule zao zimefanya vizuri na kuahidi kuendelea kushilikiana nao ili kufikia lengo la ufaulu wa hali ya juu zaidi.

"Imekuwa ni kawaida yetu kufanya vizuri hivyo sio kitu cha ajabu sana kwa matokeo haya ambayo tumeyapata na tutaendelea kufanya hivi mpaka ufaulu ufike asilimia 100" alisema Hapi.

Chapisha Maoni

 
Top