Ukitaja marais barani Afrika ambao wanapenda soka huwezi kumtoa Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye yeye ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Arsenal.
Sasa kutokana na ukaribu uliopo kati ya Rais Kagame na Viongozi wa klabu ya Arsenal huenda ukawa ni chanzo cha nchi hiyo kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitangaza nchi Kiutalii.
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na serikali ya Rwanda imeeleza kuwa Jezi za Arsenal kwa miaka mitatu itavaa jezi zenye logo ndogo mkononi zilizoandikwa ‘Visit Rwanda’ kwa lengo la kupromoti utalii.
Logo hiyo itawekwa kwa timu zote za Arsenal za wanaume na wanawake kuanzia msimu mpya wa 2018/19 unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Agosti.
Rwanda kwa mwaka inapokea watalii milioni 1.3 na kwa hatua hii huenda watalii wakaongezeka maradufu ndani ya miaka mitatu.
Chapisha Maoni