Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza |
Tume hiyo iliyojumuisha wataalam kutoka Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika ilipewa mamlaka ya kuchunguza ukiukwaji wa haki za biandamu nchini Burundi na kutoa mapendekezo juu ya uboreshaji wa haki hizo na msaada wa kiufundi katika maridhiano na utekelezaji wa mkataba wa Arusha.
Kiongozi wa tume hiyo Christof Heyns amesema wamebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na serikali huku akisema hakuna uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa habari na wamebaini hofu kubwa miongoni mwa wananchi na hata wale wa jirani, akisema hilo litafuatiliwa kwa karibu.
Heyns amesema kuwa serikali imeaonesha nia ndogo au nia ya kuzuia au kukomesha ukiukwaji hu0 mkubwa na kuongeza kuwa tangu kuanza kwa mgogoro, hakuna uwajibikaji kutoka kwa vikosi vya usalama au kundi la chama tawala cha Imbonerakure.
Chapisha Maoni