0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina.
Naibu Waziri Muungano na Mazingira Luhaga Mpina ametoa siku mbili kwa uongozi mkuu wa mamlaka ya anga nchini, TCAA, kutoa taarifa kamili za uendeshaji wa shughuli za anga katika visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na makusanyo yanayoingia serikalini.

Naibu Waziri Mpina ametoa agizo hilo wakati akiongea na Uongozi wa Mamlaka ya Anga tawi la Zanzibar, alipofanya ziara fupi katika ofisi za mamlaka hiyo katika uwanja wa kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Luhaga Mpina amesema kuwa taarifa za uendeshaji na usimamizi mzima wa makusanyo ya mapato ya mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar kulingana na ndege zinazoingia ndani na nje ya nchi kwa upande wa Zanzibar.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa kutokuwa na uwazi juu ya masuala mbalimbali ya muungano ndiyo sababu ya kuwepo dhana ya kunyonywa katika mgawanyo wa mapato kati ya Tanzania Bara na Visiwa hivyo vya Zanzibar.
Mpina amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo kurekebisha mfumo wa kukusanya data na kutaka kila ofisi iwe na takwimu kamili ya mapato yatokanayo na usafiri wa anga ili kuondoa migongano iliyopo.

Chapisha Maoni

 
Top