0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, amesema kuwa mradi wa upimaji na kuwezesha wananchi kupata ardhi utasaidia kutatua kwa kiasi kikubwa cha migogoro ya ardhi mkoani humo na kuufanya mkoa kuendelea kuwa ghala la taifa la chakula.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Dkt. Kebwe amesema mradi huo ambao unafanywa na serikali pamoja na nchi mbalimbali wahisani unalenga kutoa fursa zaidi za uwekezaji mkoani humo kwa kuweka mazingira safi ambayo yataondoa migogoro kati ya wananchi na wawekezaji au wakulima na wafugaji.
Dkt. Kebwe amesema kuwa mradi huo ambao unagharibu karibu bilioni 30 za Kitanzania mbali ya ndani ya miaka mitatu kufanikisha kila mwananchi kupata eneo lakini pia utainisha maeneo ya Kilimo, Mifugo, na maeneo mengine ya akiba bila muingiliano wa kimipaka.
Dkt. Kebwe amesema serikali inaamini kuwa watanzania kupitia mradi huo pamoja na mafunzo watakayopata kila mwananchi atakayekuwa na eneo atajua kama ni kulima alime kwa kiasi gani au mifugo awe na idadi gani ya mifugo ili asiingilie eneo la mwingine.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kuanzia katika wilaya ya Mvomero ambapo migogoro mingi imejitokeza serikali imeshaweka kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kukamilisha mradi huo kwa haraka zaidi ili kutatua migogoro inayoendelea katika wilaya hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top