0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIC Bw. Clifford Tandari.
Vijana nchini wametakiwa kuachana na mtazamo wa kutoka vijijini kukimbilia mijini kwa lengo la kutafuta maisha mazuri na badala yake wabaki katika maeneo yao huku wakichangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika kilimo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam leo katika mkutano wa pamoja alioufanya na kituo cha uwekezaji nchini TIC ambapo mkuu huyo wa mkoa amezungumzia kongamano la uwekezaji litakalofanyika mkoani humo hivi karibuni.
Clifford Tandari ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIC ambapo amewaambia waandishi wa habari kuwa sekta ya usafirishaji ndiyo inayoongoza kati ya miradi yote ya uwekezaji iliyopo mkoani Morogoro ikifuatiwa na sekta ya kilimo.

Chapisha Maoni

 
Top