0
Mashabiki wa Simba na Yanga katika dimba la Taifa
Kuelekea katika mpambano wa watani wa Jadi Simba SC dhidi ya Yanga utakaopigwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mashabiki wa soka nchini wametakiwa kulinda mali za uwanja huo ili uendelee kudumu kwa matumizi ya baadaye.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo nchini BMT Alex Nkenyenge amesema, pamoja na kuulinda Uwanja huo, lakini pia mashabiki wa soka wanatakiwa kulipa viingilio halali ili kuviwezesha vilabu kupata fedha za kuendeleza shughuli za soka nchini ikiwa ni pamoja na kutimiza malengo waliyojiwekea.
Nkenyenge amesema, vilabu vinashindwa kuendelea kutokana na kukosa mapato yanayopatikana katika michezo mbalimbali ndani ya Uwanja husika unaotumika hivyo iwapo mashabiki watazingatia viingilio vilivyowekwa watakuwa wamevisaidia vilabu kwa kiasi kikubwa.
Mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga na muendelezo wa michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara na kwa sasa Simba SC imeweka kambi yake mkoani Morogoro huku Yanga ikiwa imeweka kambi yake visiwani Pemba.

Chapisha Maoni

 
Top