Afisa habari wa klabu ya Yanga Bw. Jerry Muro
ameamua kukubali hukumu iliyoolewa dhidi yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) inayomtaka kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka
mmoja.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa instagra, Muro ame-post ujumbe unaoashiria ameamua kuukubali uamuzi huo huku akisisitiza atawa-miss mashabiki wake wa Yanga.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa instagra, Muro ame-post ujumbe unaoashiria ameamua kuukubali uamuzi huo huku akisisitiza atawa-miss mashabiki wake wa Yanga.
“Kila nikifikiria figisu za soka la Bongo aisee nachoka kabisa,
let me walk away for a while though I will be missing my fans and my people wa
kimataifa but I must walk away for a while,” ndivyo inavyosomeka post ya Jery Muro
kwenye account yake instagram.
Kamati ya nidhamu ya TFF
ilimtia hatiani Jerry Muro kwa kosa la kupinga uamuzi wa TFF na kulishambulia
kupitia vyombo vya habari shirikisho hilo la soka nchini ambapo kamati hiyo
ilitoa adhabu ya kumfungia Muro kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja
pamoja na faini ya shilingi milioni tatu za Tanzania.
Chapisha Maoni