Bi Theresa May amechukua usukani kama waziri mkuu wa Uingereza.
Akizungumza
baada ya kupokea ufungua wa makao rasmi ya waziri mkuu wa Uingereza 10 Downing
Street bi May amehakikishia washirika wake na mataifa ya muungano wa ulaya kuwa
licha ya taifa hilo kuamua kujiondoa,Uingereza
inapania kujiunga na mataifa shirika na kutekeleza wajibu wake katika muungano
wa mataifa huru duniani.Amesema
kuwa serikali yake haitanaswa na mtego wa kuwasikiza mabwenyenye walio wachache
na kusahau wananchi wa kawaida.
May amesema kuwa
serikali yake itahakikisha inawakilisha matarajio ya kila muingereza.Aliwakumbusha
wakosoaji wake maana ya jina rasmi ya chama chake ambacho ni chama cha
Conservative and Unionist.Waziri
huyo mkuu ameapa kuangamiza udhalimu wa aina yeyote ima ni kwa misingi ya
ubaguzi wa rangi jinsia ama kiwango cha mapato.Bi
Theresa May ni waziri mkuu wa 13 kuwahi kuiongoza Uingereza katika enzi ya
Malkia Elizabeth wa pili.
Malkia tayari amempa
idhini ya kuunda serikali mpya muda mchache tu baada ya kujiuzulu rasmi kwa
aliyekuwa waziri mkuu bwana David Cameron.Yeye
ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret Thatcher.
Chapisha Maoni