Na
je katika enzi hizi za simu za kisasa au Smartphone wangapi wetu wanatumia simu
za kale zisizo na touchscreen?
Haya
basi, Hayo sio maswali ya kipima joto ... la!
Rais wa Uganda Bw Yoweri Kaguta Museveni alizua kioja katika
kijiji cha Kyeirumba, wilaya ya Isingiro karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania
aliposimamisha msafara wake wa magari ili apokee simu "ya dharura".
Picha za kisa hicho zilipakiwa kwenye mtandao wa Facebook na afisa wake wa
habari Don Wanyama.
Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari
lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya
Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu
faraghani.
Mzee Museveni kama
vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia
mkono wapita njia.
Baada
ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa
wakuu serikalini.
Ilikuwa ajabu sana kwao kumuona Museveni akiwa ameketi
barabarani.
Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya
rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.
Wengine wanamkejeli
kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimkosoaa kwa kuketi barabarani.
''Kwani
hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?"
''Ni
siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.
''Ama
ilikuwa ni #Besigyexit?", wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa
kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.
...........................
Chapisha Maoni