Mshambuliaji Wilfried Bony, 27, anajiandaa kuondoka Manchester
City, huku Galatasaray wakitoa pauni milioni 3 za kumsajili kwa mkopo (Sun),
Leroy Sane, 20 anayesakwa na Manchester City, hajaiambia klabu yake ya Schalke
kuwa anataka kuondoka, wakati meneja mpya wa City Pep Guardiola akiwa tayari
kutoa pauni milioni 40 kumsajili kiungo huyo Mjerumani (Daily Star).
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumsajili
kiungo kutoka Spain, Cesc Fabregas, 29, ambaye alikuwa naye Chelsea (Daily
Mirror), Mourinho huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Newcastle, Moussa
Sissoko, 26, iwapo atashindwa kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus (Le 10
Sport), Man United wanaendelea kumfuatilia beki wa West Ham, Reece Oxford, 17
(Evening Standard), meneja msaidizi wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs,
41, atacheza katika ligi kuu ya India mwezi huu (Daily Mail).
Meneja wa Sunderland Sam Allardyce anaonekana huenda akatajwa
kuwa meneja wa England na Gary Neville kuwa msaidizi wake (Daily Mirror), dau
la pauni milioni 25 la Arsenal kumtaka beki Daniele Rugani, 21, limekataliwa na
Juventus (Calciomercato), Arsenal wako tayari kuwapa Napoli Olivier Giroud, 29,
pamoja na pauni milioni 42, ili wamsajili Gonzalo Higuain, 28 (Sun), Arsenal na
Chelsea wanamfuatilia beki wa Roma Kostas Manolas, 25 (Corriere Dello Sport).
Chelsea wana wasiwasi kuwa huenda wakalazimika kulipa zaidi ya
pauni milioni 50 kumsajili beki Kalidou Koulibaly, 25, kutoka Napoli (Evening
Standard), Real Madrid wameingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa Valencia
Andre Gomes anayefuatiliwa na Chelsea (Fichajes), Madrid wameamua kutomuuza
mshambuliaji wao, Alvaro Morata, 23, kwenda Chelsea (Daily Mail).
Liverpool na Tottenham hawajakatishwa tamaa na bei ya pauni
milioni 25 iliyowekwa kwa beki wa Kols, Jonas Hectors, 26 (Bild), Middlesbrough
waliopanda daraja wanataka kumsajili beki wa Chelsea Tomas Kalas, 23 (Daily
Express), Middlebrough pia wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Valencia
Alvaro Negredo, 30, aliyeichezea Manchester City kwa misimu miwili (Guardian).
Swansea wanataka kupanda dau kumsajili Leonardo Ulloa, 29,
kutoka Leicester, wakati wakijiandaa kwa kuondoka kwa Andre Ayew na Bafetimbi
Gomis (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Wales Hal Robson-Kanu ambaye ni
mchezaji huru amepewa mshahara wa pauni 100,000 kujiunga na Ligi Kuu ya China
(Daily Mirror)
.
Wawakilishi wa Moussa Sissoko wamemtaka meneja wa Newcastle,
Rafael Benitez, kuingilia kati mzozo kuhusu bei ya pauni milioni 35 aliyowekewa
kiungo huyo ambayo wanahisi inamzuia kuondoka (Daily Mirror), Newcastle wako tayari
kusikiliza dau la kuanzia pauni milioni 20 kumsajili Sissoko, 26, ambaye
aling’ara kwenye michuano ya Euro 2016 (Times), Marseille wataelekeza nguvu zao
kumtaka Carlos Sanchez, 30, baada ya kushindwa kumpata Idrissa Gana kutoka
Aston Villa (Birmingham Mail).
Chapisha Maoni