Watu wengi husumbuka
sana wanapoandika ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutokana na hali kwamba
herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida.
Aidha, mtindo wake
huwa mmoja.
Je, wajua unaweza
kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo
(italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza
strikethrough?
Unachohitaji kufanya
kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu
yako.
Kuweka bold
Ili kukoza rangi
kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya
nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo nyota.
Kwa mfano, ukiandika
*bold* itatokea ikiwa bold
Kuweka italiki
Ili kufanya herufi
zako kuwa za mlazo au kuwa za italiki, unahitajika kutanguliza na mstari sakafu
(underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.
Ukiandika _italics_
itatokea ikiwa italics
Kuweka strikethrough
Ukitaka kuweka alama
ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi au
kwa Kiingereza tilde (~) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.
Ukiandika
~strikethrough~ itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.
Kuunganisha
mitindo
Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake kuwa na bold na
italiki.
Utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno
lako na kuhitimisha.
Mfano,
ukiandika _*bolditalics*_ inafaa kutokea ikiwa bolditalics.
Chapisha Maoni