![]() |
Kenya imepanda hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya shirikisho la soka duniani FIFA |
Kenya imepanda hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya
shirikisho la soka duniani FIFA na kuorodheshwa katika nafasi ya 86 duniani.
Hii
ni kwa mujibu wa orodha ya FIFA inayoonesha kuwa Algeria imesalia kidedea
barani Afrika japo inaorodheshwa katika nafasi ya 32 duniani.Jamhuri
ya kidemokrasia ya Congo ndiyo inayoongoza katika kanda ya afrika mashariki na
kati.DR
Congo imeorodheshwa katika nafasi ya 59 duniani na 9 barani Afrika.Uganda
Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69 duniani
nafasi mbili mbele ya vigogo ya soka barani humu Nigeria.
![]() |
Orodha ya FIFA Tanzania 123 |
Kenya ambayo ndilo
taifa lililoimarika zaidi inaorodheshwa katika nafasi ya 86.Harambee
stars ya Kenya iliyojifurukuta na kuilaza Congo Brazzaville iliimarika hatua 43
na kuingia chini ya mataifa bora 100 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha
miezi sita.Aidha
hii ndiyo nafasi ya juu zaidi kwa Kenya tangu mwaka wa 2008.Amavubi
Stars ya Rwanda imeshuka hatua 8 na kuorodheshwa katika nafasi 111 duniani.
![]() |
Uganda Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69 duniani |
Licha ya kupanda hatua
13, Taifa Stars ya Tanzania inaorodheshwa katika nafasi ya 123Inafatwa kwa karibu na
Burundi ambayo vilevile imepanda hatua 7 na kutimia nafasi ya 125.Ethiopia ni ya 132,Sudan 142Sudan Kusini 153Mataifa ya mwisho
kabisa katika orodha hiyo ya FIFA ni mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki yaani
Djibouti, Eritrea na Somalia ambazo zote zinaorodheshwa katika nafasi ya 205.Argentina ingali
inaongoza duniani ikifwatwa na Ubeljiji.
Orodha ya mataifa kumi
bora barani Afrika
Algeria (32)
Ivory Coast (35)
Ghana (36)
Senegal (41)
Misri (43)
Tunisia (45)
Cameroon (53)
Morocco (54)
DR Congo(59)
Mali (61)
Algeria (32)
Ivory Coast (35)
Ghana (36)
Senegal (41)
Misri (43)
Tunisia (45)
Cameroon (53)
Morocco (54)
DR Congo(59)
Mali (61)
Orodha ya mataifa kumi
bora duniani
1 Argentina
2 Ubeljiji
3 Colombia
4 Ujerumani
5 Chile
6 Ureno
7 Ufaransa
8 Spain
9 Brazil
10 Italia
1 Argentina
2 Ubeljiji
3 Colombia
4 Ujerumani
5 Chile
6 Ureno
7 Ufaransa
8 Spain
9 Brazil
10 Italia
Chapisha Maoni