0
Biashara ya mazao katika moja ya soko la Dar es Salaam
Serikali imeombwa kuondoa ushuru wa mazao unaotozwa na halmashauri mbalimbali nchini pamoja na kupunguza bei ya pembejeo za kilimo, kama njia ya kupunguza gharama na bei kubwa ya vyakula kwa walaji na wanunuzi wa rejareja.

Wito huo umetolewa hii leo na wafanyabiashara kutoka masoko kadhaa jijini Dar es Salaam likiwemo Soko la Nafaka la Mapinduzi lililopo Mwananyamala, ambapo wamesema gharama hizo zimekuwa zikichangia bei kubwa ya bidhaa za vyakula kwa walaji.
EATV imeshuhudia mchele sokoni hapo ukiuzwa kwa bei ya chini ya kati ya shilingi 1,000 na shilingi 1,800 kwa kilo moja, huku wauzaji wake wakisema bei inaweza kuwa chini ya hapo ikiwa kutakuwa na maboresho katika gharama za uzalishaji.

Chapisha Maoni

 
Top