Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri |
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya wajasiriamali zaidi ya 200 yaliyoendeshwa na shirika la viwanda vidogo nchini (SIDO), kwa kushirikiana na shirika la Maendeleo la Uholanzi(SNV).
Mwanri amesema kuwa mara nyingi jamii hasa vijana wanaangamia kiuchumi kwa kukosa ujuzi, hivyo suala la utaalamu na ujuzi ni jambo nyeti ambalo vijana wengi wanapaswa kupewa elimu hiyo ili kujiendeleza na kujikwamua kiuchumi.
Mwanri amesema kwa vijana wengi wamekuwa wakilalamika na kushindwa kutumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi hivyo wayatumie mafunzo hayo waliyoyapata ya ujasiriamali ili kubadili maisha yao na familia zao kwa ujumla.
Chapisha Maoni