0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kutangaza zabuni kwa ajili ya ununuzi wa rada sita za kisasa kwa ajili ya kuboresha usimamizi na ufuatiliaji wa safari za anga nchini.

Profesa Mbarawa amesema hayo Mjini Unguja mara baada ya kukagua shughuli zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga -TCAA, Mamlaka ya Hali ya Hewa -TMA na Uwanja wa Ndege wa Zanzibar ambapo amesisitiza umuhimu wa kufata sheria katika kumpata mzabuni.
Profesa Mbarawa ameitaka TCAA kuhakikisha kwamba marubani wanaopewa vibali vya kurusha ndege nchini wanakidhi vigezo vya kimataifa ili kuufanya usafiri wa anga kuwa salama na wa uhakika.
Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume amempongeza Profesa Mbarawa kwa ushirikiano anaoufanya kati ya Wizara hizo na kusisitiza kuwa hali hiyo itaongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za Serikali na kuleta tija kwa wananchi na kuongeza kuwa ni vyema Huduma zinazopatikana Tanzinia bara zipatekane na Zanzibar ili wazanzibari nao waweze kunufaika nazo ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano kwani kwa kufanya hivyo kuleta usawa kwa wananchi wa pande zote za Muungano
Profesa Mbarawa yupo Mjini Unguja katika ziara ya kukagua taasisi zilizo chini ya wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na kubadilishana uzoefu na viongozi wa wizara hiyo (Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji) kwa upande wa Zanzibar.

Chapisha Maoni

 
Top