![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan |
Akiongea katika mkutano wa hadhara na wananchi wa wilaya hiyo amesema kuwa atawakamata akina mama watakao waruhusu wanaume kuingia katika maboma yao na kisha kufanikisha kitendo hicho na kusema serikali ya wilaya hiyo haitavumilia hata kidogo.
Akizungumza katika uzinduzi wa shule mpya katika kijiji cha lengrorit amesema wazazi na walezi wachukue fursa hiyo kuwapeleka watoto wao shule na kuacha kisingizo cha watoto kusoma umbali mrefu ambapo walikuwa wanakumbana na vitisho vya wanyama wakali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Monduli, Bw. Wiliam Sanare amesema kuwa wakazi wa eneo hilo wanapaswa kutumia fursa ya shule hiyo kuhakikisha watoto wote wanapata elimu ili kufuta ujinga na umasikini katika eneo hilo.

Chapisha Maoni