![]() |
| Ramani ya Nigeria |
Mapema Alhamisi vyombo vya habari vimeripoti kwamba wafungwa wenye ghadhabu, katika gereza la Abakaliki kwenye jimbo la Ebonyi, walianzisha ghasia kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni tatizo la uhaba wa chakula.
Serikali ilisema ilitumia mabomu ya kutoa machozi na kufyatua risasi za moto hewani kudhibiti kuenea zaidi kwa vurugu hizo.
Mkasa huo unakuja katika juma ambalo maafisa 23 wa magereza walifukuzwa kazi kutokana na kile kilichodaiwa kupanga njama za jaribio la kutorosha wafungwa.

Chapisha Maoni