![]() |
| Waziri wa Afya Ummy Mwalimu |
Akifafanua kuusiana na suala hilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa kulinda usalama na haki ya watoto nchini iliyoandaliwa na taasisi za kitaifa na kimataifa jijini Dar es salaam juu ya haki za wasichana Mhe. Ummy Mwalimu amesema sheria hiyo ikipitishwa chini ya mahakama ya rufaa itakuwa na nguvu zaidi kwani haiwezi kupingwa na chombo chachote cha kisheria hivyo kufanikisha hazma ya serikali kupiga vita mimba za utotoni.
“Tumekaa meza ya pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali kujadili suala hilo, mwana sheria mkuu wa serikali amesema kwamba dhamira yake ilikuwa ni kutoa fursa ya kesi hiyo kusikilizwa na kuamuliwa na mahakama ya rufaa, na rufaa ikishindwa ina maana hakuna chombo chochote cha chini kisheria kitakwenda kinyume na sheria hiyo” amesema
Mhe. Ummy amewahakikishia wana harakati mbalimbali, asasi za kiraia na taasisi za kimataifa kuwa serikali inadhamira ya dhati ya kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 au 15 kwa ridhaa ya wazazi kwani imekuwa na adhari nyingi katika ustawi wa watoto wa kike nchini.
Hivi karibuni mwanasheria mkuu wa serikali alikata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu ya kuitaka serikali kurekebisha sheria ya ndoa inayomtaka mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 au 15 kwa ridhaa ya mzazi hatua ambayo ilipingwa na wanaharakati wa masuala ya jinsia.
Naye Edda Sanga Mkurugenzi wa taasisi ya wanawake waandishi wa habari TAMWA amesema kutokana na tamko hilo la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuwa itaokoa mamilioni ya wanawake hasa maeneo ya vijijini ambao wameendelea kuishi katika umasikini mkubwa kutokana na adhari za ndoa za utotoni.

Chapisha Maoni