0
Binti aliyepata mimba akiwa chini ya umri wa miaka 18
Takribani watoto Millioni 3.5 wa umri wa miaka 7 mpaka 17 walionje ya shule nchini Tanzania wapo kwenye hatari ya kupata mimba za utotoni jambo ambalo linahatarisha afya zao na maendeleo yao kiuchumi.

Utafiti wa hali ya Afya na Uzazia, Mtoto na Maleria wa mwaka 2015/2016 inaonyesha idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15 mpaka 19 imeongezeka kufikia asilimia 27mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010 jambao ambalo linachangia vifo vya uzazi kwa wanawake wazazi wenye umri mdogo kati ya miaka 15 mpaka 18.
Mikoa inayoongoza nchini Tanzania kwa kuwa na tatizo hilo ni mkoa wa Katavi wenye asilimia 36.8, Mkoa wa Tabora wenye asilimia 36.5, Simiyu asilimia 32.1, Geita Asilimia 31.6 na Shinyanga ni Asilimia 31.2 hivyo jitihada za wadau katika kutoa hamasa ya elimu kwenye mikoa hiyo.
Akiongea na East Africa Television jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema wengi wa watoto hao wapatao Milioni 2 walitakiwa kuwa shule za msingi sawa na asilimia 23 na watoto wengine Milioni 1.5 walitakiwa kuwa shule za sekondari ambayo ni sawa na asilimi 41.
Mhe. Ummy amesema elimu kwa watoto wa kike humsaidia msichana kufanya maamuzi bora yake na familia yake, na manufaa ya elimu yao yanaweza kuonekana kwa watu binafsi sambamba na kucheleweshaa ndoa na Mbimba kwa wasichana wadogo.
“tunaweza kupambana na aina zote za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana hasa waishio vijijini, kuhakikisha kuwa wanakuwa na uhuru zaidi kiuchumi, kuweza kudai haki yao dhidi ya mila potofu kama ndoa za utotoni, ukeketaji na kuwalinda kikamilifu dhidi ya ndoa za utotoni” amesema
Mhe. Ummy amesema kutokana na madhara hayo serikali ya awamu ya tano inaendeleza jitihada za kufanya marekebisho ya sheria ya Ndoa ya mwaka 1977 hususani katika kifungu namba 13(1) cha sheria ya ndoa kinachoelezea kwamba umri wa mtoto wa kike kuolewa ni kuanzia miaka 15.
Ameendeleo kueleza kuwa, Sheria hiyo kupitia kifungu cha 13 (2) kinaweka mazingira kwa mtoto wa miaka 14 kufunga ndoa iwapo kuna ruhusa ya mahakama hivyo ukinzani huo wa sheria hii na sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inayosisitiza kuwa umri wa mtoto ni chini ya miaka 18.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa za utotoni hivyo tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaendelea kuunganisha nguvu kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazomkabili mtoto wa kike katika kupata elimi zinashugulikiwa.

Chapisha Maoni

 
Top