Wasanii wa muziki kutoka mkoani Arusha ambao wamejiwekea utofauti kwa kuimba mziki wenye lafudhi ya mkoa huo, Jambo Squad, wameelezea sababu ya wao kutoenda kufanya video nje ya nchi kwa sasa, kama ilivyo kwa wasanii wengi wa bongo fleva.
Wakizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jambo Squad wamesema wana kila sababu ya kuendelea kufanya kazi nchini, kwani hiyo itasaidia kutangaza tanzania kimataifa, pia bado wana watu wazuri wa kufanya kazi zao hapa hapa bongo.
"Umuhimu wa kufanya kazi ndani unajua ukizungumzia Tanzania ni nchi kubwa, kuna watu wanasafiri wanatoka nje wanakuja kushangaa huku Tanzania, kwa hiyo umuhimu wa kufanya huku ni umuhimu mkubwa sana kwa sababu hata kile kitu unachokifanya ukitoa, mtu akisikia Tanzania anataka aangalie Tanzania ikoje, anataka aone Tanzania ikoje, kwa sasa Jambo Squad hatujafikiria kwenda kushoot nje, kwnai bado tunaamini tuna madirector wazuri, tuna maproducer wazuri, kwa hiyo bado tunafanya kazi za nyumbani, ikifikia wakati tutaenda kufanya mbele", walisema Jambo Squad.
Jambo Squad waliendelea kusema kwamba pamoja na hayo, lakini pia kuna umuhimu wa kufanya kazi nje ya Tanzania, kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza conection na kusaidia kukuza mziki wa Tanzania kwenda kimataifa.
"Umuhimu wa kushoot nje upo na pia umuhimu wa kushoot ndani upo, kwa sababu unapoenda kushoot nje huwa unapanua mipaka yako kimuziki, unapata conection kibao, unakutana na wana, muziki wako unakua kimataifa", walisema Jambo Squad.
Chapisha Maoni