Chiku Keto |
Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Fleva Top 20, Chiku Keto amesema yeye binafsi haamini katika suala hilo kwani kila kitu kinakuwa kimeshapangwa, isipokuwa anamuomba Mungu asipate ujauzito kabla hajaolewa rasmi kwa ndoa.
"Wanasemaga eti kunakuwa na mimba ya bahati mbaya, lakini mi naonaga mimba zote zinakuwa planed, kwa sababu unapofanya kitu matokeo lazima yatokee, lakini namuomba Mungu isipatikane ya nje ya ndoa", alisema Chiku Keto.
Chiku Keto ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu na hatimaye kurudi na wimbo mpya wa 'Bado nawakilisha', Chiku Keto amesema suala la ndoa kwake bado, na hapendi kuzungumzia masuala yake binafsi kwa jamii kwani anaona si sahihi kufanya hivyo.
"Maisha ya kimahusiao kwenye public watu wanatakiwa kujua sana maisha yangu ya muziki sio ya mahusiano, kwa sababu mi naamini watahitajika kujua pale ambapo inapatikana ndoa, lakini kwa sasa hivi siko tayari kuzungumza eti mi nadate na flani, mi naona sio heshima, na sio heshima", alisema Chiku Keto.
Chapisha Maoni