0

Ntaganda analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngonoImage copyrightAFP
Image captionNtaganda analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono

Kamanda wa zamani waasi nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ambaye anakabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huko Hague, amasema kuwa yuko tayari kufa badala ya kuvumilia hali anayopitia sasa akiwa kizuizini kwa mjibu wa shirika la habari ya Reuters.
Bosco Ntaganda ambaye analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono na pia mauaji nchini Jamhuri ya Demokrasi Congo kati ya mwaka 2002 na 2003, alianza mgomo wa kutokula wiki iliyopita.

Ntaganda anasema hana uwezo wa kumuona mkewe na watotoImage copyrightAFP
Image captionNtaganda anasema hana uwezo wa kumuona mkewe na watoto

"Sina uwezo wa kumuona mke wangu na watoto tena katika hali nilivyo sasa. Hii ndiyo sababu imenifanya nipoteze matumani.Ndiyo sababu niko tayari kufa," Ntaganda alisema katika taarifa iliyosomwa na wakili wake.
Ntaganda alikana mashtaka yote 18 dhidi yake wakati wa kuanza kwa kesi mwaka uliopita.

Chapisha Maoni

 
Top