1
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa mifuko ya hifadhi za jamii nchini SSRA Bi Irene Isaka. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (SSRA) Bi Irene Isaka amesema marekebisho ya sheria namba 5 ya mwaka 2012 yalikwishafuta vipengele vya kujitoa kwenye baadhi ya mifuko ya jamii.

Amesema pia kuwa agizo la Bunge ilikuwa ni kuitaka serikali ijipange upya ili ilete mafao mbadala ya fao la kijitoa.
Bi. Irene ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio ilipotaka kujua ni kwa namna gani serikali imeanza kushughulikia malalamiko mbalimbali ambayo yanatolewa na baadhi ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kwakuwa SSRA ndio inayosimamia mifuko hiyo yote.
Amesema Bunge liliona dhana ya mifuko ya hifadhi ya jamii hairuhusu kuwepo kwa fao hilo hivyo kutokana na sababu za wanachama ni vema serikali ije na mpango mbadala wa kufanya tathimini ya kuweka mafao mbadala ambayo yatatolewa baada ya mwanachama wake kuacha kazi, hivyo kuelekeza mifuko ya jamii kuweka mifuko isiyofungamana na pande yoyote ya watumishi na wasio watumishi.
Amesema hakuna muswada wowote ambao tayari umepitishwa na Bunge na hata mapendekezo yaliyowasilishwa na serikali bado haijaridhia hivyo bado wanafuatilia na kupokea maoni kutoka kwenye vyama vyao na kuwataka wale wanaoendelea kupotosha jamii waache kwakuwa serikali inahakikisha inaendelea kutetea maslahi ya wanachama kwa kupata fidia kulingana na tatizo.
Wakati huohuo amesema wameanza utekelezaji wa kuwabaini wastaafu hewa ambao bado wanachukua mafao ya Serikali kinyume na sheria ya mafao inavyoekeza na tayari wameanza kuchukua hatua za kiutawala.
Amesema wengi waliogundulika kuchukua mafao kinyume cha sheria ni kutoka serikalini na tayari wamewaandikia ofisi ya utumishi kwaajii ya kuhakiki na kulinganisha malipo ya serikali, na uhakiki huo unafanywa na taasisi zaidi ya moja.

Chapisha Maoni

  1. huyu mama anatolewa sadaka kwa jambo la ajabu kabisa leo hii umunyime mtanzania mafao yake kwa kudanganya et atayachkua baada ya miaka 55 ni uongo. kwanza hadi sasa bado tunadhulumika a hyo pesa yetu, hakuna faida yoyote ile. leo wazee wetu mliowadanganya mnawalipa 80,000/= itawasaidia nini

    JibuFuta

 
Top