0
Bi Hillary Clinton
Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat Bi Hillary Clinton anapatiwa matibabu ya homa ya mapafu baada ya kukatiza ziara ya kutembelea eneo yalipokuwa yakifanyika maadhimisho ya shambulio la Septemba 11.

Daktari wake Dr. Lisa Bardack amesema mgombea huyo aligundulika kuwa na homa ya mapafu Ijumaa na kupatiwa matibabu baada ya kuonekana kuishiwa nguvu katika maadhimisho hayo jijini New York.
Daktari huyo amesema hali yake inaimarika ingawa maafisa wa kampeni wamesema kwamba mgombea huyo ameahirisha safari ya kampeni huko California kutokana na ugojwa, Ijumaa mkanda wa Video ulimuonesha mgombea huyo akisaidiwa na wasaidizi wake kuingia ndani ya gari.

Chapisha Maoni

 
Top