0

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira ya kilimo ili kuwavutia vijana wengi nchini kuwekeza katika sekta hiyo ambayo ndiyo fursa pekee inayoweza kutatua changamoto ya ajira nchini.

Wakiongea na na Kurasa katika maeneo tofauti jijini Dar es salaam, vijana hao Gilemwa Mwanashija na Anisye Kalonga wameitaka serikali kubadili mfumo wa elimu na kuwajengea uwezo vijana kujikita na uzalishaji wa aina mbalimbali za kilimo.
Naye Mshauri wa masuala ya kijamii Anton Luvanda amesema bila serikali kutatua changamoto hiyo ni ngumu kwa vijana kujishugulisha na kilimo kutokana na kushuhudia wazazi wao wakipata hasara kubwa katika kilimo licha ya kuwa kilimo kinalipa zaidi.

Chapisha Maoni

 
Top