0
Hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya moja ya gari la msafara wa Makamu wa Rais kupinduka, Nanguruwe Mtwara.
Msafara wa Makamu wa Rais wa wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo taarifa zinasema kati ya majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu Rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari lililokuwa limebeba baadhi ya waandishi wa habari walioambatana na ziara hiyo, liliacha njia na nusura lipinduke.
Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba, imekuwa ikitajwa kutokuwa na kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

Chapisha Maoni

 
Top