0
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam hatimaye imeanza ujenzi wa machinjio ya kisasa katika soko la Kawe.

Ujenzi huo unafanyika kufuatia habari kadhaa zilizorushwa na kituo hiki zikieleza malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara sokoni hapo wakilalamikia adha ya ukosefu wa huduma hiyo muhimu.
EATV imefika sokoni hapo na kukuta mkandarasi aliyeshinda ujenzi wa machinjio hayo kutoka kampuni ya Ganda Classic, akiendesha zoezi la uwekaji alama za ujenzi huku Diwani wa Kawe Muta Lwakatare pamoja na Mwenyekiti wa Soko hilo Yusuph Abdallah wakishuhudia na kupokea nyaraka za kuanza kwa ujenzi huo.
Diwani wa Kawe Bw. Muta Lwakatare amesema ujenzi wa machinjio hayo ni baadhi ya ahadi za uboreshaji wa soko alizozitoa kwa wakazi wa Kawe huku Mwenyekiti wa Soko Bw. Yusuph Abdallah akitoa wito kwa wateja kwenda kununua kitoweo sokoni hapo kwani huduma ya machinjio itapatikana ndani ya muda mfupi kuanzia sasa.

Chapisha Maoni

 
Top