0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umasikini nchini, REPOA, Dk Donald Mmari.
Wachambuzi wa masuala ya uchumi na maendeleo wamepongeza uamuzi wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wa kutoa muda zaidi wa majadiliano kabla ya kuridhia ushirikiano wa kibiashara kati ya EAC na Umoja wa Ulaya (EU).

Akizungumza na EATV, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umasikini nchini, REPOA, Dk. Donald Mmari, amesema, kiuchumi unapoingia kwenye mikataba ya namna hiyo kuna kiwango cha kodi ambacho nchi inapoteza kwa kuwa mikataba inaelekeza kupunguza ushuru katika nchi nyingine hivyo ni lazima kuangalia uwiano wa kuuza bidhaa, hivyo uamuzi wa EAC uko sahihi kiuchumi.
Amefafanua kwamba, kunapokuwa na ushirikiano mzuri wa uwekezaji kunapanua wigo wa masoko na kuongeza fursa za uwekezaji kutoka mataifa mengine, lakini lazima ushirikiano uzingatie uwiano wa pande zote ili kuwapa nafasi ya kuzalisha na kuweza kuuza bidhaa zao kwa faida.
Aidha, amesema ili kuzuia EAC isigeuzwe soko ni lazima kuongeza uzalishaji wa ndani wenye tija na kuongeza uwezo wa kushindana kwakuwa ardhi na rasilimali nyingine zipo.
Amesema kunapokuwa na soko kubwa EAC inabidi liwe na faida kwa nchi wanachama zinazozalisha bidhaa mbalimbali,kwakuwa sio kila nchi inazalisha bidhaa nyingi za kufanana na nchi nyngine hivyo ni lazima kuangalia vipingamizi vya biashara kama wakulima wa biashara wanaweza kuzalisha kwa wingi na kuleta ushindani na kutoa vikwazo ili wazalishaji kutoka nchi wanachama waweze kupata fursa za masoko.

Chapisha Maoni

 
Top