0
Daxo Chali
Producer aliye chini ya Mj Records Daxo Chali, ametoa siri ambayo huwafanya producers wengi kutoka kila mwaka na kuhit kisha kupotea kwenye game, huku akisema hiyo ni moja ya changamoto aliyojifunza.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Daxo Chali amesema kitendo cha kuwapa ofa wasanii wakubwa ya kurekodi bure ili aweze kutoka na kujulikana, kinawagharimu sana producers wachanga, kwani wakishakuwa na majina wakianza kuwachaji hela wasanii huwakimbia.
"Kitu kimoja ambacho nimejifunza most of the producers wanafanya kitu kama hicho ni kwamba ukimpa msanii mkubwa beat for free wakati unaanza, hata ukija kutoka yule mtu hawezi akakupa hela, i mean hawezi akakulipa, ndio maana unasikia kila mwaka kuna producer fulani ametoka, anahit, ana nyimbo nyingi, and then akishakuwa katika peak anapotea, because akiwa anaanza anafanya for free na hawa wasanii wakubwa, and then akishatoka anaanza kuwaomba hela, akishaanza kufanya hivyo tu basi wasanii wale wote wanapotea, so mi nimejifunza kitu hicho kabla sijatoka", alisema Daxo Chali.
Pia Daxo Chali amesema kufanyakazi na producers wakongwe kama Master J na kaka yake Marco Chali, kumemfanya ajifunze mengi kwenye game, na jinsi ya kuweka kazi zake kibiashara zaidi.
"Nashukuru Mungu my brothers Master J, Marco Chali nimejifunza vingi kutoka kwao, so ukisikia nimefanya kazi na mtu ujue sikuwa for free, otherwise iwe kazi labda imeanzia kwa Master J au kwa Marco, na haiwezi kuwa for free kuna makubaliano ambayo yapo, so sijawahi kumtumia msanii mkubwa beat ili aje afanye kazi na mimi kwa sababu siamini katika kutoka kwa style hiyo", alisema Daxo Chali.

Chapisha Maoni

 
Top