0
Nikki Mbishi
Rapa Nikki Mbishi ameahidi kuachia wimbo wake uitwao BABU TALENT hivi karibuni.

Tafsiri za wadau wa muziki ni kuwa wimbo huo unalenga kumdiss Babu Tale kwa kinachoaminika kuwa amekuwa akiitosa HIP HOP kwa kutowapa 'support' wasanii wa HIP HOP.
Tafsiri hizo za wadau zinaendelea kubainisha hiyo ndiyo sababu hata ya kuwabadilisha Madee na Dogo Janja kutoka kwenye rap, hadi sasa wanaimba.
Akipiga story na eNewz na kuulizwa kama ni kweli wimbo huo umemlenga Babu Tale, alikwepa kutoa jibu la moja kwa moja.
Nikki alisema “Hata nilivyoimba Nay wa Mitego watu ndiyo walijiongeza wakimfikiria Nay wanaemjua wao, lakini mimi nilimuimba Nay wa Mitego mwanamke”.
Nikki ameahidi kuachia wimbo huo hivi karibuni na kusema watu waupokee vile watakavyouelewa.

Chapisha Maoni

 
Top