0
Director Msafiri a.k.a Travellah
Mwongozaji wa video za muziki kutoka Kwetu Studio Msafiri a.k.a Travellah amesema kuwa video mpya ya Rayvanny "NATAFUTA KIKI" ni video iliyompa wakati mgumu zaidi kuitengeneza.


Akizungumza na eNewz Msafiri amesema video hiyo ilichukua siku 9 'kui-shoot', kwani wasanii wengi waliotajwa walikuwa wanakacha kutokea 'location'.
Pia Msafiri alionesha kushangazwa na kitendo cha Hanscana kuondoka WANENE ENT. kisa kikiwa ni kushidwa kutimiziwa ombi lake la kupewa RED CAMERA, Msafiri alidai kuwa kazi bora haitokani na ukubwa wa Camera tu bali pia uwezo na utundu wa Director/Camera Operator (mtumiaji) kuitumia.

Chapisha Maoni

 
Top