0
Darassa





Ikiwa sasa zimepita wiki tatu tu tangu Rapa Darassa ameachia wimbo wake wa 'Muziki' mpaka sasa video ya wimbo huo imeweza kutazamwa na zaidi ya watu milioni mbili kwenye mtandao wake wa 'Youtube'


Darassa anakuwa Rapa kwa kwanza kwa video yake kutazamwa na watu wengi zaidi ndani ya wiki tatu tu huku akiwazidi hata wasanii wengine wa kuimba ambao waliachia kazi katika kipindi kimoja.
Mashabiki wa muziki mzuri wamefurahia hatua ambayo rapa huyo amepiga na kumpongeza huku wengine wakisema kuwa ukifanya kazi nzuri lazima itapendwa na kupata watazamaji wengi zaidi kama ambavyo imetokea kwa Darassa na wimbo wake 'Muziki'


Chapisha Maoni

 
Top