0
Rais Maguli akiwa na viongozi wapya waliteuliwa hivi karibuni





Viongozi wapya wa CCM wameeleza fikra na mipango ya awali na namna walivyojipanga, kusimamia na kutekeleza ajenda ya mageuzi ndani ya chama hicho ambayo msingi wake ni kuirejesha CCM kwa watu.


Viongozi hao wapya ambao leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa chama hicho Dkt. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam, ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. Rodrick Mpogolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Bw. Humphrey Polepole na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Siasa na Mambo ya Nje Kanali Mstaafu Ngemela Eslom Lubinga.

Baada ya mazungumzo hayo, Polepole amesema Na Mhe. Rais ametuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba msimamo wa kufanya mageuzi kwenye Chama Cha Mapinduzi, kukirudisha kwenye misingi ambayo chama hiki kilianzishwa, yaani chama cha wanyonge na chama ambacho kinajinasibu na shida za watu, unatekelezwa.
"Ametuambia tukafanye kazi kwa bidii, Watanzania wana matumaini makubwa sana na Chama Cha Mapinduzi na sisi tumemhakikisha kwenda kuchapa kazi ili dhamira ya kujenga Tanzania mpya iweze kuakisiwa na kuletwa na CCM Mpya" amesema Bw. Polepole.


Chapisha Maoni

 
Top